SOMALIA-USALAMA

Sita wauawa katika shambulio la kujitoa mhanga Mogadishu

Hali ya usalama inaendelea kudorora kila kukicha Mogadishu, Somalia.
Hali ya usalama inaendelea kudorora kila kukicha Mogadishu, Somalia. REUTERS/Feisal Omar

Watu wasiopungua sita wameuawa Jumatatu wiki hii katika shambulizi la bomu lililotegwa katika gari mjini Mogadisho, nchini Somalia. Shambulizi ambalo limedaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shabab.

Matangazo ya kibiashara

Shambulizi hilo lililotokea Jumatatu wiki hii liliendeshwa katika majengo ya serikali mjini Mogadishu.

Shambulizi hilo lilidaiwa kutekelezwa na kundi la Al Shbab, lenye mafungamano na Al-Qaida, ambalo linajaribu kwa miaka kumi kuangusha serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jumuiya ya kimataifa.

"Gari lililokua limejaa vilipuzi liliingizwa ndani ya ofisi ya wilaya ya Hodan huko Mogadishu, bado hatujapata idadi kamili ya watu waliopteza maisha," Mohamed Nur, Mkuu wa polisi katika eneo hilo amesema.

Kwa mujibu wa mashahidi, ofisi hiyo iliteketea klabisa kwa moto baada ya mlipuko. Jengo jingine la serikali mjini Mogadishu liiliharibiwa vibaya wiki iliyopita katika hali hiyo kama hiyo.

Wanamgambo wa Kiislamu wa Al Shabaab walitimuliwa mjini Mogadishu mnamo mwaka 2011 na kupoteza udhibiti wa miji mingi, lakini bado wapo karibu na mji mkuu wa nchi hiyo.