MISRI-USALAMA

Wanajihadi 11 wauawa na polisi wa Misri Sinai

Vikosi vya ulinzi vya Misri Sinai.
Vikosi vya ulinzi vya Misri Sinai. AFP

Wanajihadi kumi na mmoja wameuawa katika mapigano na vikosi vya usalama vya Misri katika ngome yao ya Sinai (mashariki), eneo linalokabiliwa na mashambulizi ya kundi la Islamic State (IS), chanzo cha usalama kimesema.

Matangazo ya kibiashara

Mnamo mwezi Februari vikosi vya usalama vya Misri vilizindua operesheni kabambe iliyofahamika kwa jina la "Sinai 2018" kwa lengo la kuwatimua wanajihadi wa tawi la kundi la Islamic State, linaloendesha maovu yake kaskazini mwa eneo hilo.

"Magaidi kumi na mmoja wameuawa wakati wa ufyatulianaji risasi" na vikosi vya usalama huko al-Arich, mji mkuu wa Sinai Kaskazini, chanzo cha usalama kimebaini.

Operesheni ilikua inalenga kundi la wanajihadi lililokuwa limejificha "kwenye kituo cha mafuta kisiofanya kazi(...) kwa minajaili ya kuandaa vitendo vya kigaidi dhidi ya vikosi vya (usalama)," chanzo hicho kimeongeza.

Tangu rais aliyechaguliwa Mohamed Morsi kutimuliwa manmo mwaka 2013 na jeshi la Misri, mamia ya polisi na askari wameuawa katika mashambulizi ya kijihadi.

Takribani wanajihadi 300 na askari karibu 30 wamekufa tangu uzinduzi wa operesheni hiyo mnamo mwezi Februari, kulingana na takwimu rasmi.

Waandishi wa habari hawaruhusiwi kwenda peke yao huko Sinai lakini jeshi lilipanga ziara katika mji wa al-Arich mwezi Julai kwa vyombo vya habari vya kigeni.

Mashirika ya haki za binadamu yamekua yakishtumu mara kwa mara athari dhidi ya raia kutokana na operesheni hiyo dhidi ya wanajihadi.

CIA kuzindua mashambulizi dhidi ya wanajihadi Libya