ZIMBABWE-SIASA-USALAMA

Chamisa kuapishwa kuwa rais wa watu Zimbabwe

Nelson Chamisa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 25 Agosti 2018 Harare, Zimbabwe.
Nelson Chamisa (kulia) akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari tarehe 25 Agosti 2018 Harare, Zimbabwe. REUTERS/Philimon Bulawayo

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe cha MDC, kinaendelea kupata shinikizo za kumwapisha kiongozi wake Nelson Chamisa kuwa rais wa watu. Chama cha MDC kinaendelea kupinga matokeo ya uchaguzi yaliompa ushindi Rais Emmerson Mnangagwa.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa chama hicho kimepanga kumwapisha Chamisa siku ya Jumamosi. Hata hivyo Serikali ya Zimbabwe imeonya upinzani hasa chama cha MDC kufanya maandamano yoyote bila idhini.

Haya yanajiri wakati huu rais Emmerson Mnagangwa akiendelea kupanga serikali yake baada ya kuapishwa hivi karibuni.

Machafuko yanatarajiwa kushuhudiwa kati ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama iwapo tukio hilo litaendelea.

Hivi kaibuni Mahakama ya Katiba ilifutilia mbali madai ya chama cha MDC kupinga matokeo yaliyompa ushindi rais Emmerson Mnangangwa baada ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika mwezi Julai kwa madai kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.