CAMEROON-BAMENDA-USALAMA

Hali ya hatari yatangazwa Bamenda, Cameroon

Hali ya hatari imetangazwa katika mji wa Bamenda nchini Cameroon, wakati huu wanaharakati katika maeneo yanayozungumza lugha ya Kiingereza, wakiendelea kushinikiza, kutaka kuunda nchi yao inayoitwa Ambazonia.

Mji wa Bamenda unaendelea kukumbwa na maandamano kila kukicha.
Mji wa Bamenda unaendelea kukumbwa na maandamano kila kukicha. Photo via social media, not independently verified
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi wanaonekana wakipiga doria katika mji huo, baada ya serikali ya Yaounde kuchukua hatua hiyo na hali hii haifahamiki itaendelea hadi lini. Watu hawaruhusiwi kuwa nje kati ya saa kumi na mbili jioni na saa 12 asubuhi.

Wanaharakati kutoka eneo hilo wakiwa na bendera ya Ambazonia, walivamia magari na kuwazuia watu kusafiri hali iliyozua wasiwasi.

Jamii ya wa Cameroon wanaozungumza lugha ya Kiingereza ambao ni wachache wamekuwa wakiandamana karibu miaka miwli kupinga kile wanachosema kubaguliwa katika elimu na mfumo wa sheria.