LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Watu zaidi ya 100 wafariki baada ya boti mbili kuzama katika pwani ya Libya

Wahamiaji wakiokolewa katika Bahari ya Mediterania na shirika  lisilo la kiserikali la SOS Méditerranée, Juni 12, 2018.
Wahamiaji wakiokolewa katika Bahari ya Mediterania na shirika lisilo la kiserikali la SOS Méditerranée, Juni 12, 2018. Karpov / SOS Mediterranee/

Watu zaidi ya mia moja, ikiwa ni pamoja na watoto ishirini, walikufa maji baada ya boti mbili walizokuwemo kuzama katika pwani ya Libya mapema mwezi Septemba, kwa mjibu wa shirika la Madaktari wasio na Mipaka MSF.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa mashahidi waliohojiwa na wafanyakazi wa MSF, boti mbili ziliondoka pwani ya Libya Septemba 1 asubuhi, na kila boti lilikua limebeba watu 160, kwa mujibu wa taarifa kutoka shirika hilo lisilo la kiserikali.

Kwa mujibu wa MSF, kulikuwa na raia kutoka Sudan, Mali, Nigeria, Cameroon, Ghana, Libya, Algeria na Misri

Kwa mujibu wa mmoja wa manusura akinukuliwa na MSF boti moja lililokua limebeba watu 165 , ikiwa ni pamoja na watoto 20 lilipatwa na tatizo la injini na kuanza kuzama, lakini wachache tu waliweza kuokolewa.

Watu 55 pekee ndio walinusurika. Watoto zaidi ya 20 walifariki, kulingana na chanzo hicho, kilichonukuliwa na MSF.

Waathirika ni pamoja na wanawake wajawazito, watoto, na watoto wachanga, MSF imeongeza.