GHANA-UN-JAMII

Kofi Annan kuzikwa Alhamisi Ghana

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.
Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006. ©Reuters/Francis Kokoroko

Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Koffi Annan ambaye aliwahi kushinda tuzo ya Amani, anatarajiwa kuzikwa leo Alhamisi jijini Accra na tayari watu mbalimbali mashuhuri wameanza kuwasili nchini humo kushuhudia mazishi hayo.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano raia wa Ghana wamekua wakiendelea kutoa heshima zao za mwisho kwa Koffi Annan.

Hata hivyo, raia wengi wamesikitishwa na hatua ya kufungwa kabisa kwa Jeneza hilo na kutoweza kumwona Annan, aliyefariki dunia mwezi uliopita nchini Uswizi akiwa na miaka 80.

Viongozi kadhaa wa nchi wanatarajiwa kuhudhuria mazishi hayo katika makaburi ya jeshi ya Kambi ya Burma mjini Accra.

Marais na viongozi kutoka maeneo mbalimbali ya Afrika ikiwemo Icote d'Ivoire, Ethiopia na Zimbabwe watahudhuria shughuli hizo za mazishi, wakiwemo pia marais wa zamani kutoka nchi za Ujerumani, Finland na Uswizi.

Kofi Annan alihudumu kama Katibu Mkuu wa saba wa Umoja wa Mataifa kati ya 1997 na 2006.