ETHIOPIA-SIASA-USALA

Hali taharuki yaendelea Ethiopia

Polisi wapiga doria katika mtaa wa Addis Ababa, Ethiopia, Februari 21, 2018.
Polisi wapiga doria katika mtaa wa Addis Ababa, Ethiopia, Februari 21, 2018. © REUTERS

Hali ya taharuki inaendelea nchini Ethiopia, hasa katika mji mkuu wa nchi hiyo siku moja kabla ya kurudi nchini kwa kundi la viongozi wa kundi la waasi miongoni mwa vijana kutoka Oromo, moja ya kabila kubwa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Alhamisi wiki hii maafisa wa polisi walikabiliana na makundi ya vijana waliojihami kwa marungu na mawe na basi moja ya abiria ilishambuliwa kwa mawe karibu na eneo la Piazza, kaskazini mwa mji mkuu.

Ubalozi wa Uingereza uliripoti kwenye ukurasa wake wa Twitter machafuko katika eneo hilo na katika eneo la Karl (mashariki) wakati ubalozi wa Marekani, ulibaini kwenye taarifa yake kwamba "unachunguza taarifa za maandamano na machafuko huko Addis Ababa, na polisi ikitumwa kukabiliana na hali hiyo".

Sababu sahihi za makabiliano hayo hazikuelezwa hadi jana Alhamisi usiku lakini waandamanaji vijana walikua wakibebelea toleo la zamani la bendera ya Ethiopia.

Bendera hii imekua kama ishara ya maandamano ya kupinga serikali ambayo ilimlazimu waziri mkuu wa zamani Hailemariam Desalegn kujiuzulu na kupelekea kuteuliwa kwa Abiy Ahmed, kutoka jamii ya Oromo, kwenye nafasi ya waziri mkuu.

Waandamanaji walikua wakiimba: "Njooni muandamane, njooni mtetee bendera yenu".

Vyombo vya habari nchini Ethiopia vimeripoti kuwa wanaharakati kutoka jamii ya Oromo walikua walivalia nguo ambazo zilikua na maandishi yafuatayo "Oromo Liberation Front - OLF", katika maeneo kadhaa ya mji mkuu.