CHAD-USALAMA

Jeshi la Chad laendesha mashambulizi Tibesti

Helikopta ya jeshi la Chad (picha ya kumbukumbu).
Helikopta ya jeshi la Chad (picha ya kumbukumbu). AFP PHOTO / STEPHANE YAS

Jeshi la Chad limeendesha mashambulizi ya anga katika mji wa Kouri Bougoudi katika Jimbo la Tibesti, Kaskazini mwa Chad, ambapo operesheni ya kijeshi imekuwa ikiendelea tangu mwezi Agosti kwa lengo la kurejesha usalama katika eneo hilo, kwa mujibu wa jeshi la Chad.

Matangazo ya kibiashara

"Helikopta mbili zilifanya mashambulizi huko Kouri Bougoudi ambapo wakaazi wamekataa kuhama mji huo licha ya agizo la serikali," chanzo cha usalama mjini N'Djamena kimeliambia shirika la Habari la AFP.

"Mashambulizi hayo yalilenga tu rai wa kawaida, (kuna) raia wasio na hatia ambao wamejeruhiwa," mbenge mmoja wa eneo hilo aambaye hakutaja jina lake ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Kuna watu wane waliojeruhiwa ambao wamelekwa nchini Libya kupatiwa matibabu," mmoja wa wakaazi hao ameliambia shirika la Habari la AFP.

Akihojiwa na AFP, msemaji wa jeshi amesema hana taarifa.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, Chad ilianzisha operesheni kabambe ya kijeshi huko Tibesti ili "kurejesha usalama katika eneo" hilo.

Operesheni hii inakuja baada ya shambulio kubwa la waasi, ambalo ni la kwanza nchini Chad tangu mwaka 2009, shambulio lililotekelezwa mapema mwezi Agosti na kundi la waasi la CCMSR lenye makao yake makuu nchini Libya, katika mji wa Kouri Bougoudi.