DRC-RSF-VYOMBO VYA HABARI

RSF: Tuna wasiwasi kuhusu mwandishi wa habari aliyetoweka Bukavu

Mji wa Bukavu nchini DRC (picha kwa kumbukumbu).
Mji wa Bukavu nchini DRC (picha kwa kumbukumbu). Photo MONUSCO/Abel Kavanagh

Shirika la Waandishi wa Habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF) linasema lina wasiwasi kuhusu kutoweka kwa mwandishi wa habari huko Bukavu, katika mkoa wa Kivu Kusini, mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Hassan Murhabazi, mwandishi wa habari kwenye Radio Svein, amekua akiandaa kila Jumapili mjadala wa kisiasa, kipindi amcho kimekua kinawakutanisha wanasiasa mbalimbali, wachambuzi na wadua katika siasa ya DRC.

Alianza kupata vitisho baada ya kuzungumzia, katika kipindi chake, mada kuhusu mrithi wa Joseph Kabila, Emmanuel Shadari, kabla ya kutoweka Septemba 11.

Akihojiwa na RFI Arnaud Froger, mkuu wa RSF Afrika, ameelezea wasiwasi wake kuhusu jinsi gani uhuru wa vyombo vya habari unaminywa nchini DRC, huku waandishi wa habari wakifanyiwa vitisho na watu mbalimbali hata wale wanaoshikilia nyadhifa muhimu nchini.