ZIMBABWE-SIASA-AFYA

Upinzani waahirisha mkutano wake kufuatia mlipuko wa Kipindupindu Zimbabwe

Wagonjwa wakisubiri matibabu katika hospitali ya wagonjwa wa Kipindupindu huko Harare, Zimbabwe, Septemba 11, 2018.
Wagonjwa wakisubiri matibabu katika hospitali ya wagonjwa wa Kipindupindu huko Harare, Zimbabwe, Septemba 11, 2018. © REUTERS

Chama kikuu cha upinzani nchini Zimbabwe kimelitangaza leo Ijumaa kwamba kimeamua kuahirisha sherehe ya kuapishwa kwa kiongozi wake kama rais wa Watu nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Sherehe hiyo ilikua ilipangwa kufanyika Jumamosi Septemba 15 lakini kufuatia mlipuko wa kipindupindu, imeahirishwa hadi siku nyingine ambayo haikutajwa kwa mujibu wa chanzo cha upinzani ambacho hakikutaja jina lake.

"Chama cha Movement for Democratic Change (MDC) kimeahirisha sherehe iliyokua imepangwa Jumamosi wiki hii kwa mwaka wake wa 19 wa kusajiliwa kama chama cha siasa kutokana na kuzuka kwa ugonjwa wa Kipindupindu," msemaji wa MDC Jacob Mafume amesema katika taarifa ya chama hicho.

Rais Emmerson Mnangagwa, 75, ambaye amemruthi mtangulizi wake Robert Mugabe alitangazwa mshindi wa uchaguzi urais uliofanyika Julai 30 baada ya kupata 50.8% ya kura.

Mpinzani wake mkuu, Nelson Chamisa, alipata 44.3% ya kura lakini alikataa na kubaini kwamba uchaguzi huo uligubikwa na wizi wa kura.

Hivi karibuni malaka nchini Zimbabwe ilipiga marufu mikusanyiko ya umma huko Harare kwa sababu ya mlipuko wa kipindupindu ambao umesababisha vifo vya watu 25, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka wizara ya afya.