ETHIOPIA-USALAMA

Zaidi ya watu 23 wauawa katika machafuko ya kikabila Ethiopia

Waziri Mkuu wa ethiopia, Abiy Ahmed, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Agosti 25, 2018, tangu achukue mamlaka ya uongozi mnamo mwezi Aprili.
Waziri Mkuu wa ethiopia, Abiy Ahmed, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari Agosti 25, 2018, tangu achukue mamlaka ya uongozi mnamo mwezi Aprili. REUTERS/Kumera Gemechu

Machafuko ya kikabila yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 23 ndani ya kipindi cha siku mbili zilizopita karibu na mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, katika Jimbo la Oromo, shirika la Habari la serikali la ENA limeripoti.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa polisi katika Jimbo la Oromo, Alemayehu Ejigu, akinukuliwa na ENA, amesema kuwa kundi lililokuwa limejiandaa liliendesha mfululizo wa mauaji na uporaji kuho Burayu, magharibi mwa Addis Ababa, na kuua watu 23 na kusababisha watu 886 kuyatoroka makazi yao.

vikosi vya usalama vilitumwa ili kuzuia hali isiendelei kuzorota zaidi, na watuhumiwa 70 wamekamatwa, chanzo hicho kimesema.

"Waziri mkuu Abiy Ahmed amekemea vikali mauaji hayo na vitendo vya unyanyasaji dhidi ya raia wasio na hatia," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter Fitsum Arega, mkurugeni kwenye ofisi ya Waziri Mkuu.

Umati wa watu wameandamana leo Jumatatu wakipinga machafuko ya wiki hili. Wameshtumu vijana kutoka kabila la Oromo.