ETHIOPIA-USALAMA

Hali ya taharuki yaendelea Ethiopia

Wakimbizi wa ndani wakisubiri kupewa chakula katika kambi ilio karibu na Kebri Sahar kusini mashariki mwa Ethiopia tarehe 27 Januari 2018.
Wakimbizi wa ndani wakisubiri kupewa chakula katika kambi ilio karibu na Kebri Sahar kusini mashariki mwa Ethiopia tarehe 27 Januari 2018. AFP/Yonas Tadesse

Watu wenye hasira waliingia mitaani Jumatatu wiki hii na wakipinga kile walichodai kuwa ndugu zao waliuawa katika mapigano yaliyotokea mwishoni mwa juma lililopita.

Matangazo ya kibiashara

Maduka, migahawa na ofisi mbalimbali zililazimika kufungwa, huku sughuli mbalimbali, hasa usafiri katika mji wa Addis Ababa zikizorota.

Mapigano ya kikabila yaliyoibuka mwishoni mwa juma lililopita mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa, yamesababisha kuuawa kwa watu 23. Hali ambayo imepelekea mamia kwa maelfu ya raia kuandamana wakiwa wenye hasira kali, Maafisa wa Usalama wamebainisha.

Waandamani mjini Addis Ababa wamezuia barabara kuu za jiji hilo, sambamba na kufunga biashara mbalimbali wakiitaka serikali ichukue hatua muhimu kuzuia mauaji hayo.

Wakaazi wa jiji hilo wanawalaumu vijana wa kabila la Oromo kuwa walianzisha fujo katika mitaa ya mji wa Burayu ambapo walitumia visu, mawe na vyuma.

Polisi inasema zaidi ya watu 200 wamekamatwa kufuatia mapigano hayo.