ALGERIA-UJERUMANI-WAKIMBIZI-USALAMA

Ujerumani yakaribisha hatua ya Algeria kukubali kuwapokea raia wake

Kansela wa Ujerumani alipofanza ziara ya kiserikali nchini Algeria na kupokelwa na rais Abdelaziz Bouteflika Julai 16, 2008.
Kansela wa Ujerumani alipofanza ziara ya kiserikali nchini Algeria na kupokelwa na rais Abdelaziz Bouteflika Julai 16, 2008. ( Photo : Reuters )

Nchi ya Algeria imekubali kuwapokea raia wake wote wanaoeshi Ujerumani pasinakuwa na vibali, bila hata hivyo kujali idadi yao. Hayo yamesemwa na waziri mkuu wa Algeria Ahmed Ouyahia wakati wa ziara ya Kansela wa Ujerumani Angela Merkel jijini Alger.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano wa pamoja na Kansela Merkel, waziri Ouyahia amesema Algeria itawapokea watu wake bila kujali idadi wawe elfu 3 au elfu 5.

Upande wake Angela Merkel amekumbusha kwamba Ujerumani iko tayari kuwapokea wale wote ambao wako na sababu za kukimbia nchi yao, kama vile raia wa Iraq au Syria na kuwapa haki ya kueshi na uwezekano wa kufanya kazi.

Merkel ameongeza kuwa kwa wahamiaji ambao hawana vibali halali, serikali inatafuta washirika ambao wako tayari ambapo Algeria ni mmoja wapo na inapongezwa sana kwa hilo.

Kwa mujibu wa waziri mkuu wa Algeria, nchi yake imekuwa ikiendesha vita yenyewe dhidi ya wahamiaji haramu, hivyo kuafikiana na Algeria kuhusu swala hilo ni jambo la msingi.