AFRIKA KUSINI-DRC-SIASA-USALAMA

ANC: Tuna wasiwasi wa kutokea machafuko baada ya mkutano na upinzani DRC

(Kutoka kushoto kwenda kulia) Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Adolphe Muzito, Moise Katumbi na Jean-Pierre Bemba, wanasiasa wakuuu wa upinzani DRC kabla ya mkutano na waandishi wa habari Septemba 12. 2018 Brussels.
(Kutoka kushoto kwenda kulia) Vital Kamerhe, Felix Tshisekedi, Adolphe Muzito, Moise Katumbi na Jean-Pierre Bemba, wanasiasa wakuuu wa upinzani DRC kabla ya mkutano na waandishi wa habari Septemba 12. 2018 Brussels. AFP/John Thys

Chama tawala nchini Afrika Kusini cha African National Congress (ANC), kimesema kina hofu ya kuzuka machafuko nchini DRC baada ya kukutana na viongozi wakuu wa upinzani, ikiwa imesalia miezi mitatu kabla ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

"ANC imeelezea wasiwasi kuhusu hali inayoendelea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ambayo, ikiwa haitadhibitiwa haraka, kuna uwezekano nchi hii itumbukie katika machafuko makubwa," Chama cha African National Congress (ANC) kimesema katika taarifa yake iliyochapishwa na katibu wake mkuu Ace Magashule.

Taarifa hiyo ambayo ilitiliwa saini na viongozi sita wa upinzani ikiwa ni pamoja na kiongozi wa zamani wa kivita na makamu wa zamani wa rais Jean-Pierre Bemba na gavana wa zamani wa Katanga Moïse Katumbi, ambao wote wawili walitengwa kwenye uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika tarehe 23 Desemba mwaka huu.

"ANC inaunga mkono kanuni ya uchaguzi huru, wa haki, wa kuaminika na wa amani nchini DRC," ameongeza katibu wake mkuu baada ya kukutana na ujumbe wa vyama sita vya upinzani nchini DRC huko Johannesburg, Afrika Kusini.

ANC imeomba serikali ya Afrika Kusini "kushirikiana na serikali ya DRC na SADC (Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika)" kwa kuheshimu itifaki ya uchaguzi wa SADC.

Rais wa DRC Joseph Kabila amekua akisema sema amekataa nchi yoyote "kuingilia"katika mchakato wa uchaguzi ambao utamteua mrithi wa Rais Kabila.

Mwishoni mwa mwezi Agosti, serikali ya Kinshasa ilikataa uteuzi wa rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki kama "mjumbe maalum" nchini DRC, hatua iliyothibitishwa na vyombo vya habari lakini haikuthibitishwa rasmi na serikali ya Pretoria.