MSUMBIJI-USALAMA

Kumi na mbili wauawa katika mashambulizi ya wanajihadi Msumbiji

Kijiji kilichoshambuliwa cha Chitolo, Msumbiji, mnamo Julai 10, 2018.
Kijiji kilichoshambuliwa cha Chitolo, Msumbiji, mnamo Julai 10, 2018. © REUTERS

Makundi ya kijihadi yanaendelea kuhatarisha usalama katika maeneo mbalimbali nchini Msumbiji, huku raia wakiomba usalama wao uimarishwe. Baadhi ya raia wameyahama makaazi yao.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi watu kumi na wawili wa kijiji cha kaskazini mwa Msumbiji waliuawa na kumi na nne walijeruhiwa katika shambulio jipya lililohusishwa kundi la wanamgambo wa Kiislamu, ambalo limeendelea kuhatarisha usalama katika eneo hilo kwa miezi kadhaa.

Wanajihadi hao ambao kwa wiki kadhaa walikua hawaonekani, waliendesha shambulio lao siku ya Alhamisi wakitokea katika msitu unaopatikana na mkoa wa Cabo Delgado ambako wanajificha wakilenga mji wa Pequeue, sio mbali na Visiwa vinavyotembelewa na watalii wengi vya Quirimbas.

"Watu kumi waliuawa kwa risasi na wengine wawili waliuawa kwa kuchomwa moto," chanzo cha katika eneo hilo ambacho hakikutaja jina lake kimeliambia shirika la Habari la AFP.

Washambuliaji pia walichoma moto nyumba 55, chanzo hicho kimesema.