ZAMBIA-DRC-KOFFI-RHUMBA

Mahakama nchini Zambia yaagiza kukamatwa kwa mwanamuziki Koffi Olomide

Koffi Olomidé
Koffi Olomidé Seyllou / AFP

Mahakama nchini Zambia imeagiza kukamatwa kwa mwanamuziki wa Rhumba kutoka DRC Koffi Olomide kwa madai ya kumpiga mpiga picha nchini humo  miaka sita iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Hatua ya kuagizwa kukamatwa kwake imekuja baada ya mwamuziki huyo kutarajiwa kufika Mahakamani siku ya Ijumaa  kujibu mashtaka lakini hakuonekana.

Olomide alikuwa nchini Zambia hivi karibuni, na aliondoka licha ya kutakiwa  kufka Mahakamani.

Msimamizi wa mwanamuziki huyo nchini Zambia Mark Mumbalama, amesema alikuwa ameimba Mahakama kumpa muda zaidi Olominde kabla ya kuja Mahakamani lakini hakufanikiwa.

Mwanamuziki huyo amekuwa akishtumiwa kwa utovu wa nidhamu kwa kuwashambulia wanahabari na hata wanamuziki wenzake, kama ilivyoshuhudiwa nchini Kenya mwaka 2016.