NIGERIA-USALAMA

Kikosi cha wanamaji chawatambua raia waliotekwa Nigeria

Vikosi vya usalama vya Nigeria vinaendelea kuwatafuta mabaharia waliotekwa nyara.
Vikosi vya usalama vya Nigeria vinaendelea kuwatafuta mabaharia waliotekwa nyara. Ventures Africa

Mabaharia 12 waliokuwa ndani ya meli ya Uswisi, waliotekwa na maharamia katika Bahari ya Atlantic Pwani mwa Nigeria, imebainika kuwa walikuwa wanatokea nchini Ufilipino, Slovenia, Ukraine, Romania na Bosnia.

Matangazo ya kibiashara

Mabaharia hao walitekwa wakati meli yao ikitoka mjini Lagos kwenda mji mwingine wa Pwani wa Port Harcourt.

Utekaji nyara kama huu ni jambo la kawaida nchini Nigeria hasa katika eneo lenye utajiri wa mafuta la Niger Delta.

Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na kisa hiki, lakini na maharamia hao hawajazungumza chochote kuhusu mateka hawa, au kusem awanachotaka ili waweze kuachiliwa.

Kwa mujibu wa chanzo cha polisi nchini Nigeria, zoezi la kuwatafuta mabaharia hao linaendelea.