DRC-USALAMA

Watu 21 wauawa Beni nchini DRC

Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimamakaribu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmojahuko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018.
Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimamakaribu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmojahuko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, tarehe 13 Januari 2018. © AFP

Jeshi la DRC limetoa ripoti mpya ya watu 21 waliouawa na limesema limeanzisha uchunguzi kuhusu mauaji yaliyotokea huko Beni, mashariki mwa nchi hiyo. Mauaji ambayo yamehusishwa kundi la kigaidi la waasi wa Uganda la Allied Democratic Force (ADF).

Matangazo ya kibiashara

"Ofisi ya mashitaka ya kijeshi imefungua uchunguzi kuhusu mashambulizi mabaya yaliyoendeshwa na kundi la Kiislamu la ADF Beni dhidi ya wakaazi wa Beni, na kusababisha vifo vya raia 17 na wanajeshi 4," amesema Kanali Khumbu Ngoma afisa wa mashitaka katika mkoa wa Kivu Kaskazini, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Ripoti ya awali iliyotolewa Jumapili jioni ilibaini kwamba watu 18 sawa na raia 14 na askari wanne waliuawa.

Leo Jumatatu asubuhi, shughuli mbalimbali katika mji wa Beni zilizorota katika kuitikia wito wa mashirika ya kiraia kusalia nyumbani. Shule na maduka vimefungwa, huku watu waisalia makwao.