NIGERIA-USALAMA

Nigeria yaendelea kuwatafuta mabaharia 12 waliotekwa nyara na maharamia

Bunduki kubwa kivita ikiwa kwenye meli katika pwani ya Atlantiki, Nigeria, Desemba 19, 2013.
Bunduki kubwa kivita ikiwa kwenye meli katika pwani ya Atlantiki, Nigeria, Desemba 19, 2013. © REUTERS

Serikali ya Nigeria imetangaza kuwa inafanya kila iliwezalo ili kuwapata maharamia 12, nahodha, msaidizi wake, mafundi na wafanyakazi wengine wa meli ya mizigo waliotekwa nyara na maharamia mwishoni mwa juma lililopita katika pwani ya Delta nchini Niger.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya utawala na Udhibiti wa Usafiri wa majini nchini Nigeria (NIMASA) imetangaza kwamba "imeanza zoezi la utafutaji na uokoaji" kwa wafanyakazi wa Glarus, meli ya kampuni ya Uswisi ya Massoel Shipping.

Mkurugenzi Mkuu wa NIMASA, Dakuku Peterside, amesema katika mkutano na waandishi wa habari huko Lagos kuwa Mamlaka yake inafanya kazi "ili kuhakikisha kuwa mabaharia hao wanaachiliwa bila masharti".

Zoezi hili la utafutaji na uokoaji linafanyika na kikosi vha wanamaji cha Nigeria na mamlaka nyingine za usalama, amesema.

"Tatizo la uharamia katika Ghuba ya Guinea ni changamoto tunayotambua na tuko tayari kukabiliana nayo," dakuku Peterside amesema, huku akiahidi "kutovumilia hali hiyo".

Siku ya Jumamosi asubuhi, kundi la maharamia waliweza kuiteka meli ya Glarusna wafanyakazi wake wote, alisema siku ya Jumapili mmiliki wa meli hiyo.

Tukio hilo lilitokea kusini magharibi mwa Kisiwa cha Bonny, karibu na mji wa kusini mwa Port Harcourt.

Patrick Adamson, msemaji wa kampuni ya Massoel Shipping, ameliambia shirika la Habari la AFP kuwa "shambulio hilo ni la pili mwaka huu" katika bahari ya Ghuba ya Guinea.