BURKINA FASO-USALAMA

Askari nane wauawa nchini Burkina Faso

Askari wa BurkinaFaso wakati wa mafunzo wakiwa pamoja na wakufunzi wa jeshi kutoka Austria, karibu na mji wa Ouagadougo, Aprili 13, 2018.
Askari wa BurkinaFaso wakati wa mafunzo wakiwa pamoja na wakufunzi wa jeshi kutoka Austria, karibu na mji wa Ouagadougo, Aprili 13, 2018. © AFP

Askari wanne wa Burkina Faso wameuawa Jumatano wiki hii katika mlipuko wa bomu la kutegwa aridhini lililotengenezwa kienyeji karibu na Baraboulé, katika Jimbo la Sahel, wakati walikua njiani kwenda Djibo, mji mkuu wa mkoa wa Soum, Ofisi ya rais imesema.

Matangazo ya kibiashara

"Tumepewa taarifa kuwa askari 8 wa Burkina Faso wamepoteza maisha baada ya gari yao kukanyaga bomu la kutegwa ardhini lililotengenezwa kienyeji na kutegwa na maadui wa raia wetu," amesema rais wa Burkina Faso, Roch Marc Christian Kaboré.

"Gari iliyokua ikiongoza msafara majeshi, kutoka Baraboulé hadi Djibo, ilikanyaga kifaa cha kulipuka kilichotengenezwa kienyeji ," chanzo cha usalama kimeliambia shirika la habari la AFP.

Tukio hilo lililotokea "karibu na daraja" katika eneo hilo la kaskazini mwa Burkina Faso. Nchi hii maskini ya Sahel inayopakana na Mali na Niger,inaendelea kukabiliana kwa miaka mitatu na mashambulizi ya wanamgambo wa Kiislamu.

Kaboré alituma rambirambi zake kwa vikosi vya ulinzi na Usalama, familia na ndugu wa waathirika," huku akibaini kwamba "mashambulizi hayo ya kijinga na ya kusikitisha hayatozuia dhamira yetu ya pamoja ya kulinda nchi yetu, kurejesha amani na usalama kwa maslahi ya raia wa Burkina Faso. "

Siku ya Jumapili, polisi watatu waliuawa katika mapigano na watu wenye silaha karibu na Inata katika jimbo la Soum, ambapo wafanyakazi watatu wa mgodi wa dhahabu - raia mmoja wa India, mmoja wa Afrika Kusini, na mwengine mmoja wa Burkina Faso - walitekwa nyara.