AFRIKA KUSINI-USALAMA-HAKI

Thabo Mbeki ashtumu ANC kuwa chama cha watu weusi

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki akihudhuria maadhimisho ya miaka 100 ya Nelson Mandela katika Jumbala Constitution Hill huko Johannesburg, Julai 18, 2018.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki akihudhuria maadhimisho ya miaka 100 ya Nelson Mandela katika Jumbala Constitution Hill huko Johannesburg, Julai 18, 2018. © AFP

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Thabo Mbeki juma hili amekituhumu chama tawala cha ANC kwa kuachana na sera ya kutokuwa na ubaguzi na badala yake amesema chama hicho kinakuwa chama cha watu weusi peke yake kutokana na sera yake ya ardhi kiliyoamua kuchukua.

Matangazo ya kibiashara

Matamshi ya Mbeki ameyatoa wakati huu rais wa sasa Cyril Ramaphosa akidai kuwa katiba ya nchi hiyo itarekebishwa ili kuruhusu uchukuaji wa ardhi kutoka kwa wazungu bila ya kulipa fidia ili igawanywe kwa watu weusi.

Mbeki amesema chama tawala cha ANC kilipigana dhidi ya utawala wa ubaguzi wa rangi nchini humo ili kuleta usawa na uhuru kwa watu wote bila kujali rangi wala eneo mtu anakotoka.

Chapisho la Mbeki linalodaiwa kuvuja kwa uma, ameeleza kutoridhishwa na njia ambayo chama hicho imeamua kuchukua ya kuwanyang’anya ardhi kwa nguvu wazungu na kuwakabidhi raia weusi wa nchi hiyo bila malipo.

Uamuzi wa ANC kutaka kurekebisha katiba kuhusu ardhi, umesababisha kutazamwa hata na mataifa ya magharibi yaliyoonya kuiwekea vikwazo Afrika Kusini.