DRC yashtumiwa kuwafanyia ukatili wakimbizi wa ndani katika kambi ya Katanyika

Moto mkali ukiharibiwa sehemu ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Katanyika, karibu na Kalemie, katika mkoa wa Tanganyika, DRC.
Moto mkali ukiharibiwa sehemu ya kambi ya wakimbizi wa ndani ya Katanyika, karibu na Kalemie, katika mkoa wa Tanganyika, DRC. MSF / Louise Annaud / Twitter

Raia waliokuwa wanaishi katika kambi ya wakimbizi ya Katanika iliyoko kwenye jimbo la Tanganyika nchini DRC, kwa mara ya kwanza wameeleza madhila waliyofanyiwa na vyombo vya usalama wakati wa operesheni ya kuwafukuza kutoka kwenye kambi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo Serikali ya DRC inasema haijapokea taarifa zozote za uwepo wa vitendo vya unyanyasaji na ukatili wakati wa kutekelezwa kwa operesheni hiyo.

Hivi karibuni serikali ya DRC ilivunja kambi ya wakimbizi hao na kuwataka kurejea makwao, huku wakimbizi hao wakiendelea kuilalamikia serikali kwa kutumia nguvu wakati ambapo baadhi ya maeneo hali ya usalama bado ni tete.

Mashirika ya kiraia yaliilaumu serikali kwa kutumia nguvu dhidi ya wakimbizi hao, huku Bernard Biondo Waziri wa Mshikamano na Haki za Kibinadamu akisema hawajamfukuza mtu bali vurugu zilizozuka ni pale jeshi lilipokwenda kuwakamata wahalifu waliojificha kambini na silaha.