AFRIKA-G5 Sahel-USALAMA

Rais wa Mali atoa wito wa kuendelea kufadhili G5 sahel

Askari wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel katika Jimbo la In Tillit nchini Mali wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema mwezi Novemba 2017.
Askari wa kikosi cha pamoja cha G5 Sahel katika Jimbo la In Tillit nchini Mali wakati wa operesheni yao ya kwanza, Hawbi, mapema mwezi Novemba 2017. RFI / Anthony Fouchard

Viongozi wa Umoja wa Ulaya na umoja wa Afrika wameongeza shinikizo zaidi kwa wadhamini na pande zilizotia saini mkataba wa amani nchini Mali kuhakikisha wanaheshimu na kutekeleza makubaliano hayo, huku rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita akitaka kupewa fedha kuhakikisha mkataba huo unatekelezeka.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliongeza kwa mwaka mmoja mlolongo wa vikwazo dhidi ya Mali, na kutishia kuchukulia vikwazo kila mmoja dhidi ya viongozi wa makundi ya waasi wanaotuhumiwa kukiuka mkataba wa amani wa mwaka 2015.

Kando na mkutano wa umoja wa Mataifa jijini New York, waziri wa mambo ya kigeni wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian ameitaka Serikali ya Mali kuhakikisha mkataba huo wa amani unatekelezwa bila vikwazo.

Akizungumzia operesheni za kikosi cha G5 Sahel, rais wa Mali Ibrahimn Keita ametoa wito kwa nchi washirika kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa fedha zitakazosaidia uendeshaji wa kikosi hicho.

Kadri hali ya usalama inavyozidi kuzorota kwenye mipaka ya nchi zilizo ukanda wa Sahel, Afrika Magharibi, ndivyo umuhimu wa kikosi cha pamoja cha nchi tano kwenye ukanda huo kinavyozidi kupata umuhimu.

Ukanda wa Sahel unakabiliwa na mashambulizi na shida za mara kwa mara ambapo nchi tano kwenye ukanda huo ziliamua kuunda kikosi cha kukabili mashambulizi hayo, G5 Sahel,