NIGER-KIPINDUPINDU-AFYA

Watu zaidi ya 67 wafariki dunia kufuatia mlipuko wa kipindupindu nchini Niger

Afisa wa shiria la Msalaba Mwekundu akinynyuzia dawa ya kuzuia magonjwa katika eneo la Maradi, Niger, Septemba 24, 2018.
Afisa wa shiria la Msalaba Mwekundu akinynyuzia dawa ya kuzuia magonjwa katika eneo la Maradi, Niger, Septemba 24, 2018. IFRC/twitter.com

Mlipuko wa Kipindpindu umeua watu zaidi ya 67 nchini Niger, miongoni mwa wagonjwa kadhaa walioorodheshwa, hasa katikaJimbo la Maradi, karibu na Nigeria, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, ukinukuu ripoti kutoka Wizara ya Afya ya Niger.

Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya awali ya Umoja wa Mataifa ya tarehe 10 Septemba mwaka huu ilibani kwamba "watu 55 kwa jumla ya 2,752 walifariki dunia". Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Jimbo la Maradi, katikati-kusini mwa Niger, karibu na Nigeria, limekuwa ni chanzo cha ugonjwa huo, kwa vifo 55 na kesi 3,232 zilizotambuliwa.

"22%" ya wagonjwa huko Maradi, wanatoka Nigeria, ambapo ugonjwa wa Kipindupindu unaendelea kukumba baadhi ya majimbo, ripoti hiyo imeongeza. Lakini hadi sasa, wagonjwa wachache bado wamehifadhiwa katika maeneo yaliyotengwa ili kuwahudumia kumatibatbu wagonjwa bila malipo.

Wizara ya Afya imeonya kwamba janga hilo limesambaa, kwa mikoa mitatu, ikiwa ni pamoja na Dosso (kusini magharibi), Tahoua (magharibi) na Zinder (kusini-kati).