DRC-UN-USALAMA-SIASA

FARDC yashtumu makundi ya waasi kutoka nchi jirani kuhusika na maujai DRC

Mwili mtu aliyeuawa katika shambulizi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) Beni Aprili 16, 2015.
Mwili mtu aliyeuawa katika shambulizi la waasi wa Allied Democratic Forces (ADF) Beni Aprili 16, 2015. © AFP

Jeshi la DRC (FARDC) limeshtumu muungano unaojumuisha raia wa kigeni "wanaoendesha harakati zao kutoka nchi jirani" kuhusika katika mauaji ya mara kwa mara katika eneo la Beni, Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Jeshi la DRC limeshtumu "muungano wa kimataifa wa kigaidi unaojumuisha watu kutoka Uganda, Rwanda, Burundi, Kenya, Tanzania, Afrika Kusini, Msumbiji na watu wengine kutoka nchi jirani", kuhusika katika mauaji na machafuko mengine katika eneo la Beni, Uvira na Fizi.

"Waliondoka katika nchi zao kinyume cha sheria na kuingia nchini DRC kwa kujihusisha na vitendo viovu, vurugu kwa lengo la kuchochea uhasama na kutia uoga wananchi " katika mikoa hiyo ya sehemu ya mashariki mwa nchi,jeshi limesem akatika taarifa yake.

Jeshi la DRC (FARDC) limeahidi "kupambana kwa nguvu zote dhidi ya makundi hayo ya waasii hadi kuyatokomeza kabisa". Pia limeahidi "kusitisha opresheni hadi pale litahakikisha hakuna gaidi hata mmoja kwenye ardhi ya congo," taarifa hiyo imebaini.

Siku ya Jumamosi, shambulio la wapiganaji wa Allied Democratic Forces (ADF) katika mji wa Beni (Kivu Kaskazini) liliua raia 14 na askari wanne wa DRC.

Wakati huo huo, jeshi lilikuwalikiendesha mapambano dhidi ya wanamgambo wa Mai-Mai huko Fizi katika mkoa jirani wa Kivu Kusini (mashariki) na Djugu huko Ituri (kaskazini-mashariki). .

Wakaazi wa Beni ametupia lawama jeshi la DRC na kikosi cha Umoja w mataifa nchini humo (Monusco) wakisema kwamba wameshindwa wameshindwa kukomesha mashambulizi ya waasi dhidi ya raia.