SIERRA LEONE-AJALI

Nane wapoteza maisha katika ajali ya lori la kijeshi Sierra Leone

Afisa wa polisi mbele akitoa ulinzi Freetown, Sierra Leone, Machi 27, 2017.
Afisa wa polisi mbele akitoa ulinzi Freetown, Sierra Leone, Machi 27, 2017. © AP

Watu wasiopungua wanane wamepoteza maisha na wengine 30 wamejeruhiwa katika ajali ya lori ya kijeshi iliyotokea nchini Sierra Leone, msemaji wa jeshi amesema.

Matangazo ya kibiashara

Lori lilipindua lilipokuwa likishuka mlima katika mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown, na kuua askari watano wa Sierra Leone na ndugu watatu kutoka familia za wanajeshi.

Askari arobaini na jamaa wa askari aliyefariki dunia hivi karibuni walikuwa wanakwenda katika mazishi yake, wakati dereva wa lori alishindwa kudhibiti gari lake kwenye barabara ya Spur Road, na dakika chache baadaye ajali hiyo ikatokea, na kusababisha hali ya taharuki nchini humo, msemaji wa jeshi, Yayah Bangura, amesema.

"Askari watano na ndugu watatu wa askari wenzao walifariki dunia. Abiria wengine thelathini na mbili walipelekwa katika hospitali tatu" katika mji mkuu, Yayah Bangura ameongeza

Ajali ilitokea ilitokea kwenye eneo ambapo ajali nyingi mbaya zimekwishatokea, kwa mujibu wa wakaazi wa eneo la Lumley.

"Chanzo cha ajali bado hakijajulikana," amesema Bangura, huku akibani kwamba kuna uwezekano kwamba breki ilifeli.

"Miili inaendelea kuwasili na idadi ya waliopoteza maisha inaweza kuongezeka," amesema afisa wa chumba cha maiti cha hospitali ya umma ya Connaught.