AFRIKA KUSINI-USALAMA

Jeshi laombwa kuingilia kati Westbury, Johannesburg

Katika mji wa Johannesburg, Septemba 28, 2018: Wakazi wa Westbury waandamana wakidai udhibiti zaidi katika biashara ya madawa ya kulevya na usalama, baada ya kifo cha mwanamke mmoja.
Katika mji wa Johannesburg, Septemba 28, 2018: Wakazi wa Westbury waandamana wakidai udhibiti zaidi katika biashara ya madawa ya kulevya na usalama, baada ya kifo cha mwanamke mmoja. REUTERS/Siphiwe Sibeko

Wakaazi wa Westbury, moja ya kata za Johannesburg nchini Afrika Kusini, wametoa wito kwa askari kuwasaidia kutokomeza makundi ya wahalifu na makundi wafanyabiasha wa madawa ya kulevya.

Matangazo ya kibiashara

Kata hii inayopatikana Magharibi mwa Johannesburg ni eneo la watu waliozaliwa na wazazi wawili kutoa jambi tofauti (Wazungu na Weusi) na machafuko yalizuka baada ya kifo cha mwanamke moja aliyeuawa kwa risasi.

Hali hiyo ilianza wiki iliyopita wakati mwanamke mmoja, mama wa familia, mwenye watoto sita alipouawa katika mtaa mmoja wakati makundi hasimu yalikuwa yakirushiana risasi. Makundi yaliyokuwa yakipigania kuhusu udhibiti wa mauzo ya madawa ya kulevya katika eneo hilo. Tukio hilo liliwakasirikisha wakazi wa eneo hilo na siku ya pili yake, wakazi wa eneo hilo waliingia mitaani kupinga machafuko hayo ya kila kukicha, kupinga madawa za kulevya, huku wakiishushia lawama polisi kuwa ilinunuliwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.

Barabara kadhaa zilifungwa, majengo na ofisi za serikali ziliharibiwa vibaya. Kwa siku kadhaa, kulisuhudiwa makabiliano kati ya vijana wa eneo hiloi na polisi. Hali imeendelea kuwa mbaya. Waziri mwenye mamlaka ya Polisi alitembelea eneo hilo na kuahidi kuwa atayaangamiza makundi ya wafanyabiashara ya madawa ya kulevya. Pia polisi wengi walitumwa Alhamisi hii asubuhi, lakini wakaazi wa Westbury wamesema wanataka vikosi vya ulinzi.

Pia kuna mambo ya ubaguzi wa rangi katika matukio hayo. Wakazi wa Westbury, waliozaliwa na wazazi kutoka jamii mbili tofauti (Coloured), wanasema serikali haiwajali, imewatupilia. Nchini Afrika Kusini, watu kutoka jamii hiyo (Coloured), ambao ni mchanganyiko wa watu asili wa Cape, Koi na San, pamoja najamii nyingine za wahamiaji, hasa kutoka Asia wanasema kwamba wanatengwa kwa miaka mingi nchini humo.

Wanalalamika kuwa hawana msaada kwa makaazi, ajira, elimu kwa sababu sio Weusi. Na kata yao ni miongoni mwa maeneo maskini zaidi nchini Afrika Kusini ambapo ukosefu wa ajira ni moja ya matatizo makubwa yanayosababisha watu hasa vijana kujihusisha na madawa ya kulevya na makundi ya wahalifu. Hali hii inashuhudiwa Westbury, lakini pia Eldorado Park huko Soweto.