DRC-SIASA-EU-VIKWAZO

Shadary kwa EU : Niondoleeni vikwazo, vinaniaibisha

Mgombea urais wa chama tawala nchini DRC PPRD, Emmanuel Ramazani Shadary
Mgombea urais wa chama tawala nchini DRC PPRD, Emmanuel Ramazani Shadary Junior D. KANNAH / AFP

Mgombea wa urais kupitia chama tawala nchini DRC PPRD, Emmanuel Ramazani Shadary, ametoa wito kwa Umoja wa Ulaya kumwondolea vikwazo na watu wengine 14.

Matangazo ya kibiashara

Shadary amesema, vikwazo hivyo vinamwaibisha na havifai, wakati huu nchi hiyo inapoelekea kuwa na Uchaguzi Mkuu tarehe 23 mwezi Desemba.

Miongoni mwa vikwazo hivyo ni kumzuia Shadary kwenda barani Ulaya yeye pamoja na maafisa wengine akiwemo msemaji wa serikali Lambert Mende na Mkuu wa Inteljensia Kalev Mutondo.

Shadary na wenzake wamewekewa vikwazo hivyo kutokana na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo hasa baada ya maafisa wa usalama kuwavamia na kuwapiga waandamanaji wa upinzani na wale wanaomkosoa rais Kabila.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanasema kuwa, hali hii huenda ikamtatiza Shadary wakati wa kampeni kwa sababu wapinzani wake watatumia sababu hiyo kuomba kura.

Iwapo atachaguliwa na Umoja wa Ulaya ikatae kuondoa vikwazo hivyo, atakuwa rais wa DRC ambaye hataweza kwenda barani Ulaya.