RWANDA-LA FRANCOPHONE-LOUISE MUSHIKIWABO

Kagame asema ushindi wa Mushikiwabo ni wa kihistoria kwa Wanyarwanda

Aliyekuwa kiongozi wa OIF raia wa Canada Michaëlle Jean na mteule mpya kutoka Rwanda Louise Mushikiwabo. Erevan, le 12 octobre 2018.
Aliyekuwa kiongozi wa OIF raia wa Canada Michaëlle Jean na mteule mpya kutoka Rwanda Louise Mushikiwabo. Erevan, le 12 octobre 2018. LUDOVIC MARIN / AFP

Raisi wa Rwanda Paul Kagame na mkewe Jeannette Kagame wameungana na mataifa mbalimbali kumpongeza waziri Louise Mushikiwabo kufuatia kuchaguliwa kuongoza Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa, Francophonie.

Matangazo ya kibiashara

Raisi Kagame ameelezea ushindi wa Mushikiwabo kuwa wa kihistoria kwa wanyarwanda na waafrika ambao walimkubali kwa pamoja.

Aidha amewashukuru mataifa ya kiafrika na wanachama wengine kwa kumuunga mkono mgombea huyo kutoka Rwanda.

Makubaliano yalifikiwa katika kikao cha faragha cha viongozi wa nchi 84 wanachama wa Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa ambapo Bi Loiuse Mushikiwabo alisema "Nimekuja katika mkutano wa Erevan kama Mnyarwanda, kutoka Afrika, naondoka kama mmoja wa viongozi wa Francophonie.''

Waziri Mkuu wa Armenia Nikol Pachini, amemuahidi Kaibu Mkuu mpya wa OIF kuwa nchi yake na nchi wanachama watamuunga mkono kwa kipindi cha miaka minne ijayo.

Katika hotuba yake iliyodumu dakika chache, Louise Mushikiwabo amekiri kwamba ameipokea habari hiyo kwa "furaha nyingi", na "shukrani". Amesema akishukuru waliomteua kuchukuwa nafasi hiyo.