DRC-JOSEPH KABILA-LUBUMBASHI

Maandamano ya upinzani yapigwa marufuku nchini DRC

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Joseph Kabila REUTERS/Eduardo Munoz

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wamewauzia wanasiasa wa upinzani, kufanya mkutano wa hadhara katika mji wa Lubumbashi, ngome ya Moise Katumbi ambaye amezuiwa kurudi nyumbani,

Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wa upinzani walitarajiwa kutumia mkutano huu, kupinga matumizi ya mashine za kupigia kura, kuelekea Uchaguzi Mkuu mwezi Desemba.

Uongozi wa mji wa Lubumbashi umesema mkutano huo umefutwa kwa sababu za kiusalama, huku wanasiasa kama mgombea urais Martin Fayulu, aliyekuwa tayari amewasili katika mji huo akisema ameshangazwa na hatua hii.