NIGERIA-SIASA-HAKI

Buhari achukua hatua mpya tata dhidi ya rushwa

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Septemba 28, 2018.
Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, Septemba 28, 2018. REUTERS/Darren Ornitz/File Photo

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amechukua hatua mpya ili kupambana na rushwa, ikiwa imesalia miezi minne kabla ya uchaguzi wa urais. Maafisa zaidi ya hamsini wanaoshtumiwa kuhusika na madai ya rushwa wamewekwa kwenye orodha ya watuhumiwa ambao wanatakiwa kufuatiliwa kwa karibu.

Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa ofisi ya rais, watu hao pia watazuiwa kuondoka nchini mpaka pale kesi zao zitashughulikia. Majina ya watu hao hayajawekwa hadharani, lakini watu wengi wanaohusika na madai hayo wanaonekana ni kutoka upande wa upinzani. Njia ya kupambana na rushwa wakati kesi kuhusu watu hao zinaendelea kuchukuwa muda, ofisi ya rais wa Nigeria imesema. Wanasheria wa baadhi ya wanasiasa wa upinzani wengine, wamepinga dhidi ya hatua ambayo inahatarisha uhuru wa watu kutembea.

Kulingana na taarifa ya ofisi ya rais, idara ya Uhamiaji na vyombo vingine vya usalama vinawafuatilia kwa karibu angalau watu 50 wanaoshtumiwa kashfa hiyo. Watu hao watazuiliwa kuondoka nchini mpaka pale kesi yao itakuwa imeshughulikiwa.

"Shutma yoyote ya rushwa inapaswa kuthibitishwa katika mahakama. Isipokuwa tu kesi hizo zimechelewa. Baadhi ya kesi zinadumu miaka 10 au hata miaka 15. Na kesi nyingi kuhusu rushwa hazishughulikiwi vilivyo. Kwa sababu watu hutumia fedha walizoiba.

Hatua hizi zinakuja ikiwa imesalia miezi minne kabla ya uchaguzi wa urais. Hata hivyo upinzani umeendelea kukosoa hatua hizo ukubaini kwamba zinalenga pekee wanachama wake.