BOKO HARAM-NIGERIA-UGAIDI

Mfanyakazi wa Shirika la Msalaba mwekundu auawa nchini Nigeria

Kundi la Boko Haram nchini Nigeria
Kundi la Boko Haram nchini Nigeria REUTERS/Emmanuel Braun

Serikali ya Nigeria imethibitisha kuuawa kwa mfanyakazi wa Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu ICRC siku ya Jumatatu, baada ya kutekwa na kundi la kigaidi la Boko Haram maeneo ya Kaskazini Mashariki mwa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Mfanyakazi huyo ambaye ni muuguzi, Hauwa Leman, mwenye umri wa miaka 24, alikuwa mmoja wa wafanyakazi watatu wa kibinadamu waliokamatwa mwezi Machi mwaka 2018, wakati wa shambulio lililotekelezwa kwenye eneo hilo, maafisa wa usalama wamesema.

Taarifa zaidi zinasema kuwa wapiganaji hao wa Boko Haram wamekuwa wakitishia maisha ya wafanyakazi wa mashirika ya kutoa misaada kwa madai kuwa wanashirkiana na serikali ya Abuja.

Kundi la Boko Haram linaendelea kuwa tishio kwa watao misaada nchini humo, pamoja na raia wa kawaida kwa muda mrefu sasa.

Maelfu ya watu wamepoteza maisha, wengine kujeruhiwa kutokana na mashambulizi ya kundi hilo la kigaidi.