DRC-EBOLA-AFYA

Ebola yaendelea kusababisha vifo Mashariki mwa DRC

Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018.
Maafisa wa afya wakibeba mwili wa mgonjwa wa Ebola ambao hajathibitishwa huko Mangina, karibu na Beni, mkoa wa Kivu Kaskazini, Agosti 22, 2018. AFP/John Wessels

Shirika la afya duniani WHO linalitaka Baraza la Usalama la Umoja kupitisha bajeti zaidi ili kusaidia kukabiliana na maambukizi ya uginjwa hahtaribwa Ebola, hasa Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Shirika hilo linasema maambukizi hayo hayajafikia kiwango cha kutisha na kuathiri maeneo mengine duniani.

Wito huu umekuja, wakati huu WHO ikisema kuwa, idadi ya watu waliopoteza maisha ni 144 kwa mujibu wa ripoti ya shirika la Afya Duniani (WHO) ya tarehe 17 Oktoba 2018.

Takwimu kutokana na mlipuko uliopo sasa wa Ebola nchini DRC, unaonyesha kwamba kati ya watu 10 walioambukizwa Ebola 6 hufariki.

Kumeshuhudiwa ongezeko la visa vya Ebola katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo na mzozo unaoendelea, Kupoteza imani kwa jamii katika maeneo yalioathirika, yote haya yanatatiza jitihada za kudhibiti ugonjwa huo.

Mapigano katika eneo hilo yanafanya kuwa vigumu kudhibiti ugonjwa huo.

Wakati huo huo Uganda, Rwanda, Burundi na Sudani kusini zimetakiwa kuchukua tahadhari ya haraka kutokana na kusambaa kwa ugonjwa huu, kwasababu hali inaweza kubadilika wakati wowote kuanzia sasa.