NIGERIA-USALAMA

Amri ya kutotembea usiku yatangazwa Kaduna, Nigeria

Polisi wakipiga doria katika Jimbo la Kaduna, baada ya vurugu.
Polisi wakipiga doria katika Jimbo la Kaduna, baada ya vurugu. Reuters

Mamlaka nchini Nigeria hapo jana zimetangaza makataa ya saa 24 kwenye mji wa Kaduna baada ya kushuhudiwa mapigano kati ya vijana wa Kiislamu na Kikristo ambapo watu 55 waliuawa.

Matangazo ya kibiashara

Gavana wa jimbo la Kaduna, Nasir El-Rufai ameandika kwenye ukurasa wake wa kijamii wa Facebook kuwa Serikali yake imetangaza makataa ya kutotembea usiku ili kurejesha hali ya utulivu.

Mwishoni mwa juma mji wa Kasuwan kwenye jimbo la Kaduna umeshuhudia vurugu kubwa baada ya vijana wa jamii ya Hausa ambao ni Waislamu kukabiliana na vijana wa Adara ambao ni wakristo katika soko moja baada ya kutofautiana kuhusu uendeshaji wa shughuli zao.

Awali watu wawili waliripotiwa kufa katika soko kabla ya vijana wa Adara kuvamia makazi ya watu wa Hausa na kuanza kuchoma moto nyumba zao na kuua watu zaidi.

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametoa wito wa utulivu na kuwaonya vijana wanaojaribu kutatiza hali ya usalama kwenye eneo hilo.