COMORO-SIASA-USALAMA

Hali ya utulivu yarejea Comoro

Askari wa Comoro wakipiga doria katika mji mkuu wa Anjouan, MutsamuduOktoba 19, 2018.
Askari wa Comoro wakipiga doria katika mji mkuu wa Anjouan, MutsamuduOktoba 19, 2018. YOUSSOUF IBRAHIM / AFP

Raia wa kwenye kisiwa cha Comoro hii leo wameanza kurejea katika shughuli zao za kawaida baada ya siku 6 za makabiliano kati ya wanajeshi na waasi waliokuwa na silaha.

Matangazo ya kibiashara

Vurugu zimeshuhudiwa kwenye wilaya ya Mutsamudu mjini Anjouan ambako watu wenye silaha walikuwa wanakabiliana na wanajeshi, vurugu ambazo zinazidisha hofu kuhusu mustakabali wa nchi hiyo ambayo imewahi shuhudia mapinduzi kadhaa ya kijeshi.

Hali ya kisiasa inakumbwa na sintofahamu kwa miezi kadhaa nchini Comoro, ambapo Rais Azali Assoumani hivi karibuni alichukuwa hatua ya kukamatwa kwa wanasiasa wa upinzani.

Miongoni mwa wanasiasa wa upinzani waliokamatwa ni pamoja na rais wa zamani wa rasi hiyo Abdallah Sambi, ambaye anashtumiwa kuhusika katika madai ya rushwa. Bw Sambi ambaye ni kiongozi wa chama cha upinzani cha Juwa, ni kutoka mji wa Anjouan.

Joto la kisiasa limeendelea kupanda nchini Comoro baada ya mamlaka ya Rais Azali Assoumani kupewa uwezo zaidi kupitia kura ya maoni, ambapo kura ya Ndiyo ilishinda kwa 92,74% ya kura, huku upinzani ukisusia.