Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Mji wa Beni waendelea kukumbwa na hali ya sintofahamu

Raia wa mji wa beni waendelea kulalamikia ukosefu wa usalama.
Raia wa mji wa beni waendelea kulalamikia ukosefu wa usalama. ©RFI/Sonia Rolley
Ujumbe kutoka: RFI
1 Dakika

Wakaazi wa mji wa Beni na vitongoji vyake, mashariki mwa DRC wanaendelea kupinga kile wanachosema kuwa mauaji yamekithiri, huku wakilaumu vikosi vya usalama na ulinzi kushindwa kudhibiti usalama.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumapili polisi kwenye mji huo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya raia walioandamana kupinga mauaji yanayoendelea kushuhudiwa kwenye eneo hilo.

Maandamano haya yalifanyika baada ya kuuawa kwa watu 11 na kutekwa kwa watu wengine 15 wakiwemo watoto.

Mashambulizi haya si ya kwanza kushuhudiwa kwenye eneo la mashariki mwa nchi hiyo

Wataalamu wa masuala ya siasa wanaona kuwa itakuwa vigumu mauaji hayo kukoma ikiwa wafadhili wa makundi hayo hawatakemewa au kukamatwa.

Baadhi ya wachambuzi wa siasa za nchi za maziwa makuu waliozungumza na idhaa hii, wanasema kuwa kuendelea kuwepo kwa makundi haya ni sehemu ya mipango ya baadhi ya nchi kutaka kutatiza mchakato wa uchaguzi wa desemba 23 mwaka huu.

Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.