Mushikiwabo afanya ziara yake ya kwanza baada ya kuchaguliwa kama Katibu Mkuu wa OIF

Louise Mushikiwabo (picha ya kumbukumbu, Septemba 2018).
Louise Mushikiwabo (picha ya kumbukumbu, Septemba 2018). LUDOVIC MARIN / AFP

Majuma mawili baada ya kuchaguliwa kuwa katibu mkuu wa Jumuiya ya nchi zinazo zungumza lugha ya Kifaransa Francophonie, Louise Mushikiwabo ameanza ziara katika mataifa ya Afrika yaliomuunga mkono kwa ajili ya kutoa shukrani baada ya kufaanikisha zoezi la kuchaguliwa kuiongoza taasisi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

Ziara yake ya kwanza imemfikisha jijini Brazaville nchini Congo ambako amekutana na viongozi mbalimbali na kuahidi kutekeleza ahadi zake wakati wa muhula wake ambao utaanza mwezi Januari.

Aidha, amesema haitasahau nchi yake ya Rwanda.

"Ni wazi kwamba katika kutekeleza majukumu yangu nchi yangu haitatengwa. Rwanda ni nchi yenye lugha nyingi. Umuhimu wa lugha ya Kifaransa - kwa uhakika - utakuwa kipaumbele, "amesema Louise Mushikiwabo.

Baada ya kuzungumza na waandishi wa habari Louise Mushikiwabo amepands ndege na kuelekea katika mji wa Oyo ambako amekwenda kukutana na rais wa Congo Brazaville Dennis Sassou Nguesso.