DRC-EBOLA-AFYA

Ebola yaua watu zaidi ya 186 Mashariki mwa DRC

Chanjo ya kuzuia kuenea kwa Ebola yandelea kutolewa kwa wakazi wa wialaya ya Beni na vitongoji vyake.
Chanjo ya kuzuia kuenea kwa Ebola yandelea kutolewa kwa wakazi wa wialaya ya Beni na vitongoji vyake. REUTERS/Kenny Katombe

Mtoto mchanga na mama yake walioambukizwa hivi karibuni virusi vya Ebola Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamekamilisha idadi ya watu 298 walioambukizwa ugonjwa huo ambao umeua watu zaidi ya 186, maafisa wa afya nchini DRC wamesema.

Matangazo ya kibiashara

Kesi hizi mbili mpya za maambukizi zilizothibitisha huko Mabalako, katika wilaya ya Beni, ni mwanamke anayeishi huko Beni na mtoto mchanga wake wa wiki mbili, "kulingana na jarida la kila siku la Wizara ya Afya ya DRC ya siku ya Jumapili tarehe 4 Novemba 2018.

Mtoto huyo na mama yake wameanza kuhudumiwa katika kituo maalumu cha wilaya ya Beni kilicoanzishwa na serikali ili kuzuia kusambaa kwa ugonjwa huo na kutoa huduma, kulinagana na jarida la kila siku la Wizara ya Afya ambalo pia limebaini pia kwamba "Watu 81 ya waliokuwa wameambukizwa virusi vya Ebola wamepona".

"Jumla ya watu 298 wameambukizwa virusi vya Ebola katika kanda hiyo, ikiwa ni pamoja na kesi 263 ambazo zimethibitishwa".

"Tangu kuanza kutolewa chanjo mnamo Agosti 8, 2018, watu 26,135 wamepewa chanjo, ikiwa ni pamoja na 13,825 katika wilaya ya Beni," timu inayokabiliana na ugonjwa huo imesema katika taarifa yake.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), Dk. Tedros Adhanom Ghebreyesus, na Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayehusika na shughuli za amani Jean-Pierre Lacroix watafanya ziara ya pamoja nchini DRC tarehe 05 hadi 09 Novemba, Florence Marchal, msemaji wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC (Monusco) ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mlipuko wa kwanza wa ugonjwa wa Ebola uliripotiwa huko Yambuku Kaskazini Mashariki mwa DRC mwaka 1976, na uliua watu 224.