Wagombea katika uchaguzi Madagascar waendelea kunadi sera zao

Rais wa mwisho, mgombea kwa muhula wa pili Hery Rajaonarimampianina, wakati wa mkutano wake katika uwanja wa Coliseum, Antananarivo, Novemba 4, 2018.
Rais wa mwisho, mgombea kwa muhula wa pili Hery Rajaonarimampianina, wakati wa mkutano wake katika uwanja wa Coliseum, Antananarivo, Novemba 4, 2018. RIJASOLO / AFP

Raia wa Madagascar tarehe saba mwezi huu watapiga kura katika uchaguzi mkuu wa urais ambao utashuhudia marais watatu wa zamani wa taifa hilo wakichuana.

Matangazo ya kibiashara

Taifa hilo litafanya uchaguzi huku likiwa na kumbukumbu mbaya ya mizozo ya kisiasa, huku mzozo wa karibu ni ule wa mwanzoni mwa mwaka huu baada ya rais Hery Rajaona-rimampia-nina kutaka kubadili sheria za uchaguzi.

Rais Hery Rajaomarimampianina atachuana na rais wa zamani Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina ambao kwa nyakati tofauti waliongoza taifa hilo kabla ya kuondolewa madarakani kwa mapinduzi na maandamano.

Mwishoni mwa juma hili lililopita, vigogo hao watatu wa siasa za Madagascar, ambao ni marais wa zamani wa nchi hiyo waliendesha kampeni yao ambayo inamalizika Jumatatu, Novemba 5. Baada ya Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina, ilikuwa ni zamu ya Hery Rajaonarimampianina kukusanya wafuasi wake siku ya Jumapili, Novemba 4.

Mbele ya maelfu ya watu waliokusanyika kwenye uwanja wa Coliseum, Hery Rajaonarimampianina aliomba muda zaidi kwa wafuasi wake.

Kati ya wagombea 35 ambao bado wamejidhatiti katika uchaguzi huo, walifanya kampeni zao jana Jumapili katika maeno tofauti ikiwa ni pamoja na mchungaji Mailhol,Kiongozi wa kanisa la Apocalypse ambalo lina waumini milioni mbili.