Wanajihadi 19 wauawa Misri
Imechapishwa:
Wanajihadi 19 waliokuwa wamehusishwa na tukio la kigaidi la kuwashambulia wakiristo saba wa dhehebu la Coptic nchini Misri, wameuawa.
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo imesema, washukuwa hao waliuawa katika makabiliano makali na maafisa wa usalama. Shambulio hilo lilitokea siku ya Ijumaa (Desemba 29)
Misri imeendelea kusumbuliwa na makundi ya kigaidi, huku Wakiristo wa dhebu la Coptic wakiwa hatarini.
Siku ya Ijumaa watu wasiopungua saba waliuawa katika shambulio dhidi ya kanisa la Coptic kusini mwa Cairo, nchini Misri.
Shambulizi hili linathibitishwa kuwa waumini wa Kanisa la Coptic bado wanaendelea kulengwa na Waislamu wenye msimamo mkali. Makanisa matatu yamelengwa tangu mwezi Desemba 2016. Wakristo 100 waliuawa katika mashambulizi hayo.