SUDAN-KIIR-USALAMA-SIASA

Salva Kiir ateuliwa kuwa mratibu wa mgogoro wa Sudan

Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Rais wa Sudan Kusini, Salva Kiir, ameteuliwa kuwa mpatanishi katika mazungumzo ya amani kati ya Khartoum na waasi wa maeneo ya Darfur (magharibi), Kordofan ya Kusini (kusini) na Blue Nile (kusini) nchini Sudan.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatatu Mshauri wa masuala ya usalama wa Salva Kiir, Tut Kew, aliwaambia waandishi wa habari kwambarais Salva Kiir amekubali "kuwa mratibu wa mazungumzo kati ya serikali ya Khartoum na waasi nchini Sudan."

"kazi ya Salva Kiir iutaanza wiki ijayo huko Juba, ambapo wajumbe wa upinzani na wajumbe wa serikali wataanza mazungumzo ya amani," alisema.

Nchi ndogo zaidi duniani, Sudan Kusini ilipata uhuru kutoka Sudan mwaka 2011 baada ya miaka 22 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Tangu wakati huo, mgogoro kati ya serikali ya Khartoum na waasi wa Sudan People Liberation Movement (SPLM-N, kutoka SPLM ya Salva Kiir) katika maeneo ya Blue Nile na Kordofan Kusini umekuwa ukiendelea.

Juba na Khartoum walikuwa wakishtumiana kila mmoja kusaidia waasi.

Vikao kadhaa vya mazungumzo kati ya serikali ya Sudan na waasi havikuzaa matunda yoyote.

Waasi wa SPLM-N wanashirikiana na waasi wa Darfur, eneo kubwa kama Ufaransa, linalokabiliwa na machafuko tangu mwaka 2003 kati ya vikosi vya Sudan na waasi kutoka jamii ya watu wachache ambao wanaona kuwa wametengwa na serikali kuu ya Khartoum.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, vita nchini Darfur vimesababisha vifo vya watu 300,000 na zaidi ya milioni 2.5 ambao wamelazimika kutoroka makazi yao, ingawa kiwango cha machafuko kimeshuka kwa kiasi kikubwa katika miaka ya hivi karibuni.