GAMBIA-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yaunga mkono demokrasia nchini Gambia

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian akiambatana na Rais wa Gambia Adama Barrow katika ikulu Banjul, Novemba 5, 2018.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa Jean-Yves Le Drian akiambatana na Rais wa Gambia Adama Barrow katika ikulu Banjul, Novemba 5, 2018. Clare Bargeles / AFP

Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, amefanya ziara ya kikazi nchini Gambia ili "kuonyesha uungwaji mkono wa Ufaransa kwa kudumisha demokrasia" nchini humo, karibu miaka miwili baada ya aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Yahya Jammeh, kulazimika kwenda uhamishoni.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa ziara yake iliyodumu saa chache, Waziri wa Mambo ya Nje wa Ufaransa amezungumza na Rais Adama Barrow, ambaye amemrithi Bw Jammeh tangu mwezi Januari 2017. Yahya Jammeh alitawala nchi ya Gambia kwa muda wa miaka 22.

Ufaransa imetoa msaada wa euro milioni 50 kwa nchi hii ndogo ya Magharibi mwa Afrika inayozungumza Kiingereza kwa muda wa miaka minne. Hatua hii ya Paris imeifanya Ufaransa kuwa mfadhili wa kwanza kwa nchi hii "katika sehemu ya mpango wake wa maendeleo ya kitaifa, kulingana na taarifa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa (Quai d'Orsay).

Ufaransa imejikubalisha kufadhili miradi katika sekta ya kilimo na upatikanaji wa maji ya kunywa.

Hii ni ishara kuwa Ufaransa inaendelea kuimarisha uwepo wake nchini Gambia, ambapo pia alitembelea juma lililopita Mwanamfalme Charles, mrithi wa uongozi wa Uingereza.

"Ili Gambia iweze kulinda usalama wake vilivyo, ni lazima ifuate njia ya maridhiano ya kitaifa, ambayo inafuata kwa sasa," amesema Bw Le Drian.

Waziri wa anatarajia kuhudhuria leo Jumanne nchini Senegal Mkutano wa 5 wa kimataifa kuhusu Amani na Usalama barani Afrika na kukutana kwa mazungumzo na Rais Macky Sall.

Nchini Senegal, Bw Le Drian anatarajiwa kuzungumzi kuhusu miradi mikubwa, kama vile treni ya mwendo kasi katika ukanda huo (TER), ambayo uzinduzi wa sehemu ya kwanza umepangwa mapema mwaka 2019, pamoja na mabadiliko ya tabia nchi.