CAMEROON-USALAMA-SIASA

Biya awaonya waasi kuweka silaha chini

Rais wa Cameroon Paul Biya.
Rais wa Cameroon Paul Biya. © AFP PHOTO / REINNIER KAZE

Rais wa Cameroon Paul Biya kwa mara ya kwanza amekiri kukabiliwa na changamoto ya kurejesha imani na utulivu kwenye eneo la kaskazini mwa nchi hiyo ambako raia wake wanazungumza lugha ya kiingereza.

Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati wa kuapishwa kwake siku ya Jumanne, Rais Biya amewaonya waasi wa eneo hilo wanaoendesha vitendo vya kihalifu, akiipa Serikali yake kushughulikia mzozo wa eneo hilo akiwataka waasi hao kuweka silaha chini ama wakabiliwe na nguvu ya vyombo vya sheria.

Matamshi yake yamekuja wakati ikiwa ni siku mbili tu zimepita tangu waasi wa eneo hilo kuwateka wanafunzi zaidi ya 79.

Mpaka sasa hakuna kundi lolote, nchini Cameroon ambalo limejitokeza kudai kuwateka watu 80 wakiwemo wanafunzi zaidi ya 79 kutoka eneo linalozungumza lugha ya Kiingereza.

Serikali ya Cameroon imewashatumu wapiganaji wanaotaka kujitenga kwa maeneo yanayozungmza lugha ya Kingereza, kuwa wamehusika.

Wakati huo huo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guteress ametoa wito wa kuachiliwa huru kwa wanafunzi hao.