MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa urais Madagascar: Wagombea 36 na wapiga kura milioni 10 wapiga kura

Antananarivo, Novemba 6, 2018.
Antananarivo, Novemba 6, 2018. MARCO LONGARI / AFP

Wapiga kura milioni kumi wanapiga kura Jumatano hii Novemba 7 nchini Madagascar kwa duru ya kwanza ya kumchagua rais wao mpya kati ya wagombea 36, ikiwa ni pamoja na marais wa zamani wanne, mawaziri wa zamani watatu, wachungaji, na mwanamuziki mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Ushindani mkali ni kati ya wagombea watatu, marais wote wa zamani: Marc Ravalomanana, Andry Rajoelina na Hery Rajaonarimampianina.

Marais hao wa zamani wamekuwa wakitumia nguvu kubwa kuwashawishi wapiga kura. Wamekuwa wakipiga kampeni nchi nzima kwa kutumia helikopta, wakisambaza fulana katika mikutano yao pamoja na kutoa matangazo katika vyombo vya habari vya taifa.

Uchaguzi ambapo ni kipimo kwa nchi hii inayokabiliwa mara kwa mara na mgogoro wa baada ya uchaguzi.

Rais anayemaliza muda wake Henry Rajaonarimampianina anawania pia tena awamu ya pili madarakani.

Kampeni za uchaguzi nchini humo zilijawa na utata kufuatia matumizi ya fedha ya wagombea wakuu watatu kati ya 36 wanao wania nafasi hiyo.

Ravalomanana aliitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 2002 hadi 2009 alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na Andry Rajoelina, ambaye wakati huo alikuwa Meya katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo.

Viongozi wote hao walipigwa marufuku kuwania kiti hicho tena mwaka 2013 kufuatia shinikizo kutoka jumuia ya kimataifa,