MADAGASCAR-UCHAGUZI-SIASA

Zoezi la kuhesabu kura laendelea Madagascar

Zoezi la uhesabuji kura katika maeneo ya chini mwa mji mkuu wa Madagascar, Novemba 7, 2018.
Zoezi la uhesabuji kura katika maeneo ya chini mwa mji mkuu wa Madagascar, Novemba 7, 2018. © RFI/Sarah Tétaud

Kura zinaendelea kuhesabiwa nchini Madagascar, baada ya Uchaguzi wa urais kufanyika siku ya Jumatano. Uchaguzi huu ni kipimo kwa nchi hii inayokabiliwa mara kwa mara na mgogoro wa baada ya uchaguzi.

Matangazo ya kibiashara

Wagombea 36, waliwania wadhifa wa urais lakini, ushindani ni kati ya marais watatu waliowhi kuongoza taifa hilo, Hery Rajaona, Marc Ravalomanana na Andry Rajoelina.

Wapiga kura milioni kumi waliitikia uchaguzi huo ambao ulifanyika kwa duru ya kwanza.

Rais anayemaliza muda wake Henry Rajaonarimampianina anawania pia tena awamu ya pili madarakani.

Kampeni za uchaguzi nchini humo zilijawa na utata kufuatia matumizi ya fedha ya wagombea wakuu watatu kati ya 36 wanao wania nafasi hiyo.

Ravalomanana aliitawala nchi hiyo kuanzia mwaka 2002 hadi 2009 alipoondolewa madarakani kwa mapinduzi yaliyofanywa na Andry Rajoelina, ambaye wakati huo alikuwa Meya katika mji mkuu wa nchi hiyo Antananarivo.

Viongozi wote hao walipigwa marufuku kuwania kiti hicho tena mwaka 2013 kufuatia shinikizo kutoka jumuia ya kimataifa,