ETHIOPIA-HAKI-UCHUNGUZI

Miili mia mbili yagunduliwa katika kaburi la pamoja Ethiopia

Wakazi wa Jimbo la Oromia waliwakosa ndugu zao wakati wa machafuko katika jimbo hilo.
Wakazi wa Jimbo la Oromia waliwakosa ndugu zao wakati wa machafuko katika jimbo hilo. REUTERS/Tiksa Negeri

Polisi nchini Ethiopia wanasema wamegundua kaburi la pamoja, likiwa na miili 200 kwenye mpaka wa majimbo ya Somalia na Oromia. Watu wengi walitoroka makazi yao mwaka mmoja uliopita kutokana na ghasia katika eneo hilo.

Matangazo ya kibiashara

Inaaminiwa kuwa, watu hao walipoteza maisha baada ya kuzuka kwa mapigano ya kikabila katika Jimbo la Somali.

Polisi inafanya uchunguzi juu ya madai ya ukatili yaliyofanywa na rais wa zamani wa Ethiopia katika jimbo hilo.

Aliyekuwa rais wa Jimbo la Somali, Abdi Mohammed, alilazimika kujiuzulu kwenye nafasi hiyo, mnamo mwezi Agosti mwaka huu na kuwekwa mbaroni akisubiri hukumu dhidi ya madai ya kuchochea mapigano ya kikabila karibu na mpaka wa Somalia na mikoa ya Oromia.

Inashukiwa kuwa, polisi wanaofahamika kama Liyu walihusika na mauaji hayo kwa amri ya Abdi Mohammed.