GABON-SIASA-AFYA

Gabon: Ali Bongo Ondimba anaendelea kutekeleza majukumu yake kama rais

Rais Ali Bongo Ondimba, hapa ilikuwa Januari 29, 2018, huko Addis Ababa, Ethiopia.
Rais Ali Bongo Ondimba, hapa ilikuwa Januari 29, 2018, huko Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Tiksa Negeri

Ofisi ya rais nchini Gabon imetoa taarifa mpya kuhusu hali ya afya ya rais wa nchi hiyo Ali Bongo Ondimba. Rais wa Gabon alipelekwa hospitali nchini Saudi Arabia, ambako alishiriki katika mkutano wa Davos.

Matangazo ya kibiashara

Hivi karibuni taarifa mbalimbali, ambazo serikali ya Gabon inadai kuwa ni uzushi, zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii zikieleza kuwa Ali Bongo yuko katika hali mahututi. Taarifa mpya kutoka ofisi ya rais nchini Gabon, iliyochapishwa Jumapili hii, Novemba 11, inasema kuwa afya yake imeimarika kwa kiasi kikubwa na anaendelea kutekeleza majukumu yake kama rais wa Gabon.

Wananchi wa Gabon waliendelea kutokuwa na taarifa yoyote kuhusu hali ya afya ya rais wao kwa muda wa wiki mbili. Hakujakuwa na taarifa zozote rasmi kuhusiana na afya ya rais tangu matangazo ya mwanzo yalipotolewa Oktoba 28 kuhusiana na afya yake kwamba amechoka na anahitaji mapumziko. Msemaji wa rais, Ike Ngouoni, amesema kuwa Ali Bongo Ondimba alilazwa katika hospitali ya Kingo Faysal baada ya kuonekana kuwa ana "uchovu mkubwa".

Habari zilizosambaa kuhusiana na rais huyo mwenye umri wa miaka 59, zinasema kuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa Kiharusi.

Rais Ali Bongo alichukua madaraka ya kuiuongoza Gabon kutoka kwa baba yake Omar Bongo mwaka 2009, ambaye aliiongoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 40.