DRC-UPINZANI-SIASA

Martin Fayulu ateuliwa kuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais DRC

Martin Fayulu (katikati) aliteuliwa rasmi kuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 nchini DRC. Uamuzi ulioafikiwa huko Geneva na viongozi wakuu saba wa upinzani, Novemba 11, 2018.
Martin Fayulu (katikati) aliteuliwa rasmi kuwa mgombea wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 nchini DRC. Uamuzi ulioafikiwa huko Geneva na viongozi wakuu saba wa upinzani, Novemba 11, 2018. Fabrice COFFRINI / AFP

Hatimaye upinzani umeafikiana na kumteua Martin Fayulu kuwa mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi ujao wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 23 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo imefikiwa katika mazungumzo ya siku tatu yaliyowajumuisha viongozi wakuu saba wa upinzani huko Geneva, nchini Uswisi. Mazungumzo ambayo yaliwezeshwa na wakfu wa Kofi Annan.

Uteuzi wa Martin Fayul, kiongozi wa chama cha upinzani cha Ecidé umewashangaza wengi kwani hakuwa miongoni mwa watua mbao walikuwa wanapewa nafasi ya kuchukuwa na fasi hiyo.

Martin Fayulu, mwenye umri wa miaka 61, si maarufu katika siasa ndani na nje ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wala hakuwa anafahamika miongoni mwa wanasiasa wakuu wa upinzani nchini humo.

Hata hivyo alishiriki kwenye mstari wa mbele katika maandamano makubwa yaliyoikumba DRC tangu mwaka 2015 na kuonekana mmoja kati ya watu wanaopinga rais Joseph Kabila kuwania kwa muhula watatu.

Wagombea wa upinzani ambao walikuwa wameorodheshwa kuwania urais huko Geneva ni pamoja na Felix Tshisekedi, Vital Kamerhe, Martin Fayulu na Freddy Matungulu.

Wanasiasa hao wa upinzani walikuwa na muda, hadi mwishoni mwa wiki hii kukubaliana ni nani kati yao atapambana na mgombea wa chama tawala Emmanuel Ramazani Shaddary.

Mara ya mwisho kwa wanasiasa hawa kukutana ilikuwa ni miezi kadhaa mjini Pretoria nchini Afrika Kusini na wakakubaliana kuwa na mgombea mmoja.

Felix Tshisekedi, mmoja wa viongozi wa kuu wa upinzani aliokuwa anapewa nafasi kubwa ya kuchukuwa na fasi hiyo, amepongeza hatua hiyo na kubaini kwamba hivi karibuni wataanza zoezi la kuhamasisha wafuasi wao kumuunga mkono na kumpigia kura Martin Fayulu katika uchaguzi wa Desemba 23.