DRC-UPINZANI-SIASA

PPRD na washirika wake: Hatuna wasi wasi na uteuzi wa Fayulu

Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani wa DRC na Mbunge wa PPRD Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23.
Waziri wa zamani wa Mambo ya Ndani wa DRC na Mbunge wa PPRD Emmanuel Ramazani Shadary ni mgombea wa wengi katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23. Junior D. KANNAH / AFP

Chama tawala nchini DRC na washirika wake wamesema hawana wasiwasi na uteuzi wa Martin Fayulu kama mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa urais wa Desemba 23 katika kumirthi Rais Joseph Kabila kwenye uongozi wa nchi hiyo.

Matangazo ya kibiashara

"Vyama vinavyounga mkono utawala wa Rais Kabila vimepokea kwa mikono miwili uteuzi mbunge Martin Fayulu kama mgombea wa pekee wa upinzani," wakili Tunda Kasende, naibu katibu mkuu wa chama cha rais cha PPRD ameliambia shirika la Habari la AFP.

"Hatuna wasiwasi na uteuzi huu,na ninajiuliza kama kweli atakuwa na muda wa kujiandaa dhidi ya mgombea wetu ambaye ana timu inayofanya kazi kwa miezi kadhaa," ameongeza Bw Tunda.

Wakati huo huo wafuasi wenye hasira dhidi ya uteuzi wa Martin Fayul wameandamana Jumatatu wiki hii mbele ya makao makuu ya vyama viwili vya upinzani.

Hayo yanajiri wakati baadhi ya wafuasi wa chama cha UDPS "wamechoma moto picha za Felix Tshisekedi wakiacha zile za baba yake, Étienne Tshisekedi. Polisi wanajaribu kulinda usalama vilivyo, hapakuwa na tukio lolote baya shughuli zinaendelea kama kawaida, "msemaji wa polisi Kanali Pierrot Mwanamputu ameliambia shirika la Habari la AFP.

Mashahidi kadhaa waliohojiwa na AFP wanasema waliona matairi ya yalichomwa moto mbele ya makao makuu ya vyama vya UDPS na UNC cha spika wa zamani wa Bunge Bunge, Vital Kamerhe .

Fayulu anatarajiwa kukabiliana na Emmanuel Ramazani Shadary, mgombea wa wengi, tarehe 23 Desemba, akipeperusha bendera ya muungano mpya wa vyama vya upinzani ulioundwa Geneva kwa jina la Lamuka (kwa Lingala) ikimaanisha Amka.

Baada ya kuahirishwa mara mbili tangu mwaka 2016, uchaguzi wa urais umepangwa kufanyika Desemba 23mwaka huu.