DRC-UPINZANI-SIASA

Upinzani kushiriki uchaguzi ukiwa pamoja DRC

Kutoka kushoto kwenda kulia: Jean-Pierre Bemba, Adolphe Muzito, Alan Doss (wakfu wa Kofi Annan), Martin Fayulu, Freddy Matungulu, Felix Tshisekedi, Moise Katumbi na Vital Kamerhe. Geneva, Novemba 11, 2018.
Kutoka kushoto kwenda kulia: Jean-Pierre Bemba, Adolphe Muzito, Alan Doss (wakfu wa Kofi Annan), Martin Fayulu, Freddy Matungulu, Felix Tshisekedi, Moise Katumbi na Vital Kamerhe. Geneva, Novemba 11, 2018. Fabrice COFFRINI / AFP

Hatimaye upinzani unatarajia kujitokeza katika uchaguzi ujao wa Desemba 23 ukiwa umeungana baada ya Martin Fayulu kuteuliwa kuwa mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa rais wa Desemba 23.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imefikiwa na viongozi wakuu saba wa upinzani, baada ya siku tatu za mazungumzo huko Geneva, Uswisi, yaliyowezeshwa na wakfu wa Kofi Annan.

Uteuzi wa Martin Fayul, kiongozi wa chama cha upinzani cha Ecidé umewashangaza wengi kwani hakuwa miongoni mwa watu mbao walikuwa wanapewa nafasi ya kuchukuwa na fasi hiyo hasa Felix Tshisekedi wa chama cha UDPS na Vital Kamerhe wa chama cha UNC.

Hata hivyo Muungano wa vyama vinavyounga mkono chama tawala cha PPRD , FCC, vinavyoendelea kumuunga mkono Joseph Kabila, ambaye hatowania katika uchaguzi ujao wa urais mwaka huu, umejizuia kuzungumza kuhusu uteuzi wa Martin Fayulu kama mgombea pekee wa upinzani katika uchaguzi wa Desemba 23.

Akihojiwa kwa njia ya simu, Waziri wa Mawasiliano wa DRC, Lambert Mende, amejizuia kuzungumza kuhusu uteuzi huo akisema . "Hatuna tabia ya kujihusisha katika masuala ya wengine. Kwa hivyo hatuna maoni yoyote kuhusu uteuzi huo, "amesema msemaji wa serikali.

Bw Mende ameongeza kwamba: "Nadhani ni matokeo yanayowahusu wenyewe. Hayatuhusuna hatuna maoni ya kuhusu suala hilo. Tunasubiri tarehe ya Desemba 23 raia waamue. "